Jumatatu 10 Agosti 2026 - 16:05
Waumini wa Mombasa Kenya Waadhimisha Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (as)

Hawza/ Uongozi wa AhlulBayt Assembly of Kenya umeungana na waumini katika eneo la Kisauni, Kaunti ya Mombasa, kushiriki katika maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (as), katika matembezi maalumu yaliyolenga kuhuisha kumbukumbu ya mapambano, kujitolea na msimamo wa kishujaa wa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matembezi hayo yaliyofanyika siku ya jana tare 25 Safar 1448 AH, (9 Agosti 2026), yalianzia katika Hospitali ya Sayyidah Fatma, Mlaleo, na kuhitimishwa katika Madrasat Zainul Abidin, Bilima, huku waumini wakitembea pamoja kwa moyo wa mshikamano na mapenzi juu ya Imam Hussein (as).

Katika tukio hilo, waumini walibeba ujumbe wa kuendeleza urithi wa Imam Hussein (as), ambaye alisimama kidete mbele ya dhuluma na akatoa uhai wake kwa ajili ya kuilinda haki, utu na maadili ya Uislamu.

Ushiriki wa uongozi wa AhlulBayt Assembly of Kenya katika maandamano hayo uliendelea kuonesha umuhimu wa kuhuisha mafundisho ya Karbala na kuyafanya kuwa sehemu ya maisha ya Waislamu wa vizazi vyote.

Arubaini ya Imam Hussein (as) si kumbukumbu ya tukio la kihistoria pekee, bali ni fursa ya kurejesha katika mioyo ya waumini maana ya ujasiri, kujitolea, kusimama upande wa haki na kukataa kuwa mnyenyekevu mbele ya dhuluma.

Kwa hatua zao hizo, washiriki wa maandamano walisisitiza kuwa Karbala bado inaishi katika dhamira za watu wanaoamini katika haki, na kwamba ujumbe wa Imam Hussein (as) utaendelea kudumu katika zama zote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha